NOVENA YA MT.RITHA WA KASHIA SIKU YA 6
Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho
Mtakatifu. Amina.
Nafahamu kwa
sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa na wingu zisiweze kufika katika
kiti chako cha enzi. Dhambi zangu ni sababuya adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri
wa kuelekeza sauti yangu kwa YESU. Kwakua mara nyingi sikuthamini huruma yake.
Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki. Mkono wake wa haki umenielekea.
Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha wake kwani nimegubikwa na huzuni
kubwa. Pasipo na matumaini nayalilia madhambi yangu.
Niambie
Mtakatifu Ritha, Je, niendelee kukata tamaa? Hapana. Bwana wetu YESU KRISTO
amekuteua kuwa mtetezi wake mwenye nguvu
ili uniombee kwa Yesu wangu aliye juu,msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia
safi ya kumtotendea dhambi tena.
Kwa uamuzi huu
thabiti,wa midomo yamgu na moyo wangu,nakuelekea wew. Eee Mtakatifu mtenda
miujiza,uniombee kwa Bwana Yesu fadhila ambazo nazihitaji sasa ( hapa omba hitaji lako unalotaka
kumuomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita) Katika muda huu wa uchovu mkubwa,huzuni
na kuachwa pweke, Ee Rita, neno lako kwa Yesu litafungua huruma na msamaha
wake. Sema neno na Yesu atakusikia.
Baba Yetu 3, Salamu Maria 3 na Atukuzwe
Baba 3.
Kwa njia ya
Mtakatifu Rita ~ homa, madonda na
tauni,viini vya maradhi mbalimbali mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia
vipofu,viziwi,bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa maombezi
yako : radi tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utukufu wako mitego
yote ,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukuza jia
lako. Unawasaidia
vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sanana wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi : Umemtia alama ,Ee Bwana
mtumishi wako Rita.
Wote : Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE :
Ee Mungu,
uliyekubali kutawadha Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi
akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.
Tunakuomba kupitia maombezi yake ,neemaza kusamehe adui zetu na kutafakari
maumivu ya mateso yako,ili tupate tuzo uliotuahidia kwa wapole na wanaoteseka.
Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia…….
(ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment