Litania Ya Huruma ya Mungu
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie.
Kristu utuhurumie –
Kristu utuhurumie.
Bwana utuhurumie – Bwana
utuhurumie.
Kristu utusikie – Kristu
utusikilize.
Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie Mwana
Mkombozi wa dunia Mungu – utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu – utuhurumie Utatu
Mtakatifu Mungu mmoja –utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo
sifa kuu ya Muumba wetu ~Tunakutumainia
[KIITIKIO:
Tunakutumainia]
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa
Mwokozi wetu.
Huruma ya Mungu iliyo
upendo usiopimika wa Roho Mtakasa. Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la
Utatu Mtakatifu
Huruma ya Mungu iliyo
ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi.
Huruma ya Mungu
iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni. Huruma ya Mungu
iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote. Huruma ya Mungu
inayotujalia maisha ya kutokufa.
Huruma ya Mungu
inayotukinga na adhabu tunazostahili. Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika
taabu, unyonge na maumivu ya dhambi zetu.
Huruma ya Mungu
inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu. Huruma ya Mungu
inayofurika kutoka katika majeraha ya Kristu.
Huruma ya Mungu
inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu. Huruma ya Mungu
iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma. Huruma ya Mungu
iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki. Huruma ya Mungu inayopatikana
katika mafumbo ya Sakramenti Takatifu.
Huruma ya Mungu
inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio.
Huruma ya Mungu
inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho. Huruma ya Mungu
inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika kuwatakatifuza wenye
haki.
Huruma ya Mungu
inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu.
Huruma ya Mungu chemchemi
ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka. Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote
wenye uchungu moyoni.
Huruma ya Mungu iliyo
tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tamaa.
Huruma ya Mungu iliyo
mwenzi wa daima na popote wa watu wote. Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea
neema zake.
Huruma ya Mungu iliyo
amani yao wanaokufa. Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa
toharani.
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa
watakatifu wote.
Huruma ya Mungu iliyo
taji la watakatifu wote.
Huruma ya Mungu chemchemi
ya miujiza isiyokauka. Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu
katika kuikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu, ~ Utusamehe Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu
unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma katika kila adhimisho la Sadaka ya
Misa Takatifu, ~ Utusikilize Ee Bwana. Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi
za dunia kwa njia ya huruma yako isiyo na mwisho ~ Utuhurumie.
Kiongozi: Bwana
utuhurumie –
Wote: Kristu utuhurumie,
Bwana utuhurumie.
Kiongozi: Huruma anana za
Bwana zi juu ya kazi zake zote –
Wote: Huruma za Bwana
nitaziimba milele.
Tuombe:
Ee Mungu uliye na huruma
isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo wako hazina mipaka. Tunakusihi
ututazame sisi watu wako huku duniani na kutuongezea huruma yako tena na tena,
ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata mara moja, haidhuru tukumbane na
majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima kuzielekea na kuzishika amri
zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayo ndiyo huruma
yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa
Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na Roho Mtakatifu, kwa pamoja
mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
Comments
Post a Comment