Posts

Showing posts from September, 2025

LITANIA YA MOYO MTAKATIFU WA YESU

      Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie Utatu Mtakatifu Mungu mmoja Utuhurumie Moyo wa Yesu Mwana wa Baba wa Milele Utuhurumie Moyo wa Yesu uliotungwa na Roho Mtakatifu mwilini mwa Mama Bikira Maria Utuhurumie Moyo wa Yesu ulioungana na Neno wa Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu ulio na utukufu pasipo mfano Utuhurumie Moyo wa Yesu, hekalu takatifu la Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu, hema la Yule aliye juu Utuhurumie Moyo wa Yesu tanuru lenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, nyumba ya Mungu na mlango wa Mbingu Utuhurumie Moyo wa Yesu, tanuru yenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, chombo cha haki na upendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaojaa upendo na wema Utuhurumie Moyo wa Yesu, kilindi cha fadhila zote Utuhurumie ...

Litania ya Bikira Maria

Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie. Kristo utuhurumie. Kristo utuhurumie. Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie. Kristo utusikie. Kristo utusikilize Baba wa mbinguni, Mungu, utuhurumie. Mwana Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie. Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie. Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie. Kiitikio: Utuombee Maria Mtakatifu, Mzazi Mtakatifu wa Mungu, Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira, Mama wa Kristu, Mama wa neema ya Mungu, Mama mtakatifu sana, Mama mwenye usafi wa moyo, Mama usiye na doa, Mama usiye na dhambi, Mama mpendelevu, Mama mstaajabivu, Mama wa shauri jema, Mama wa Mwumba, Mama wa Mkombozi, Bikira mwenye utaratibu, Bikira mwenye heshima, Bikira mwenye sifa, Bikira mwenye enzi, Bikira mwenye huruma, Bikira amini, Kikao cha haki, Kikao cha hekima, Sababu ya furaha yetu, Chombo cha neema, Chombo cha heshima, Chombo bora cha ibada, Waridi lenye fumbo, Mnara wa Daudi, Mnara wa pembe, N...

LITANIA KWA MT RITA WA KASHIA

Bwana Utuhurukie, Kristo Utuhurumie, Bwana Utuhurumie, Kiitikio ”Utuhurumie” Baba wa Mbinguni, Mungu, Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu, Roho Mtakatifu, Mungu, Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,   Maria Imakulata Mama wa Mungu …………………….. Kiitikio ”Utuombee” Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka Maria, Malkia wa Watakatifu wote Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita …………………….. Kiitikio ”Utuombee” Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni …………………….. Kiitikio ”Utuombee”   Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu: Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu: Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako: Mt Rita, mpenda upweke: Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo: Mt Rita, kielelezo cha upole wote: Mt Rita, kielelezo cha mke mwema: Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu: Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli: Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia: Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa: Mt Rita, kioo cha utii; Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa; Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka; Mt Rita, shahid...

NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU KWANZA

Kwa jina la Baba,na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Mtakatifu Rita   mfanya miujiza,uniangalie kwa macho yako yenye huruma,mimi ninaye teseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu umezungukwa na miiba. Yaonr macho yangu, ee Mtakatifu Rita,kuwa hayatoki machozi tena kwani machozi mengi yamenitoka! Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu? Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu wa jina hilo, kwa kunijalia toka kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba    hitaji    lako    unalotaka    kumwomba Mungu    kupitia    Mtakatifu    Rita). Kila mtu anasifia utakatifu wako. Kila mtu anasimulia maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa njia yako. Je,mimi tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uni...

NOVENA MT. RIRHA WA KASHIA SIKU YA 2

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita wa Kashia.   Naona njia ya maisha yako imejaa majaribu na miiba mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua moyo wako vipande vipande. Ee Rita uliye kweli shahidi wa maumivu makali. Uliyeonja tone kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu makali. Nafikiria juu ya moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa maombezi yako   (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita). Wewe unajua maana ya moyo unaovuja damu. Unajua pia kifodini cha roho. Umeumizwa sana na kuteseka sana. Kwa njia ya mateso hayo nakuomba unisaidie katika mahangaiko yangu. Jesi kweli kwamba wakati huu mgumu, Bwana wetu Yesu ametuandalia njia ya kujipatia neema; kupitia miujiza ambayo binadamu wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi yako wakafanikiwa? Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako. Ninakutumainia, Ee Mta...

NOVENA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 3

Kwa jina la Baba,na la Mwana,na la Roho Mtakatifu.Amina Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa mapumziko,huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu,najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Ritha,unaye ng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za kanisa katoliki,natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini,kwa hamu nangojea,kupata kile nikiombacho   (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungi kupitia Mtakatifu Ritha) Nifikshie ombi langu kwa Yesu wa msalaba.Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopata majaribu,kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa,uliyomtolea Mungu wana wako,ukiomba wasinajisi...

NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 4

  Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina Ee Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana,na wakili wa waliokata tamaa.Hizi ni sifa safi zenye kujaa tumaini kwa roho zenye kujaribiwa na uchungu.Kwako wewe Mtakatifu Rita wa kashia,ambaye wakati tunapojikuta pweke katika maisha yetu,tunapozungukwa na huzuni na kifo,wewe watujia kama mtunza bustani kutoka mbinguni kutuletea ndani ya mioyo yetu   iliyokauka tumaini na maji yaliyo hai. Ee tumaini la moyo wangu ulikauka kutokana na msongo mkubwa   wa huzuni;uzito wa maafa umenielemea,mashaka yananiogofya na sijui nielekee wapi kutafuta msaada ninaohitaji.kwako wewe Rita mwema,ninakuamini sana na kukutegemea;nakujia nikiwa na uhakika utanisikiliza. Kwa nguvu ya maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,natumaini kusikilizwa katika ombi langu   (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita) Jionyeshe tena kuwa u mwenye nguvu na huruma.Nithibitishie pia kuwa ni kweli kama wafuasi...

NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 5

  Kwa jina la baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ewe mchumba mpendwa wa Yesu, Mtakatifu Rita wa Kashia; nakuja kwako tena. Nipo miguuni pako. Navutwa na wema wako kwa Roho zenye kutaabika na kusumbuka. Unaona moyo wangu ulivyo pondwapondwa kwa magumu ya dunia hii. Sipati tena tabasamu la thanani, Roho yangu imevamiwa na mashaka mabaya. Imani imetetereka na mshituko wa kukata tamaa kama msituko wa kifo unapiga miayo miguuni pangu. Nielekeze, Ee Mtakatifu mpendwa nifanye nini katika mazingira haya ya kutisha? Nishauri nimwendee nani katika hali ya hatari katika maisha yangu. Kama kweli wewe ni Mtakatifu wa hali zote za kukatisha tamaa, njoo unisaidie kwani najisikia ninepotea. Nakuja kwako wewe ambaye kila mara wawahurumia wanaoteseka. Nakuja kwako unisaidie. Je, hutanionea huruma kutokana na hali yangu? Mtakatifu Rita najua u mwema sana. Najua hivyo , ndio maana najiweka mikononi mwako kwa moyo wangu wote ili unijibu kwa njia ya Yesu, lile ombi langu ambalo kwa iman...

NOVENA YA MT.RITHA WA KASHIA SIKU YA 6

  Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Nafahamu kwa sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa na wingu zisiweze kufika katika kiti chako cha enzi. Dhambi zangu ni sababuya adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri wa kuelekeza sauti yangu kwa YESU. Kwakua mara nyingi sikuthamini huruma yake. Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki. Mkono wake wa haki umenielekea. Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha wake kwani nimegubikwa na huzuni kubwa. Pasipo na matumaini nayalilia madhambi yangu. Niambie Mtakatifu Ritha, Je, niendelee kukata tamaa? Hapana. Bwana wetu YESU KRISTO amekuteua kuwa   mtetezi wake mwenye nguvu ili uniombee kwa Yesu wangu aliye juu,msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia safi ya kumtotendea dhambi tena. Kwa uamuzi huu thabiti,wa midomo yamgu na moyo wangu,nakuelekea wew. Eee Mtakatifu mtenda miujiza,uniombee kwa Bwana Yesu fadhila ambazo nazihitaji sasa ( hapa omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita) Katik...

NOVENA MT. RITHA KASHIA SIKU YA 7

Kwa jina LA Baba, nala Mwana, nala Roho Mtakatifu . AMINA. Ee mpedwa Rita, ambaye maisha yako yalikuwa yahuzuni. Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu makali. Naomba sala zangu, uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo wako mpole ili uweze kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote uliionesha kwa Jiran, maneno ya aman na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa watu wote vinivute kukuelekea wewe uliye katika mbingu na unakoishi na kuwa mwombezi wa watu wote waliokata tamaa. Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo kinarudi nyuma, vipofu wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza wanaponyeshwa na ulemavu wote wa roho na mwili unaondoka kabisa. Je! Nipo peke yangunjsiyefarijiwa na maombezi yako? Sitaamini wala siwezi kuamin hivyo. Nam naamini kwa dhati usimamizi wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ninamatumaini makubwa kuwa nitapata amani, moyoni wang, utulivwana fadhila ninazoomba nitajaliwa,  [ hapa   omba hitaji lako unalotaka kum...

NOVENA YA MT. RITHA KASHIA NOVENA SIKU YA 8

  Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mt. Amina Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana,ninapotafakari paji la uso wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka ktk taji la miiba la Yesu Kristo, mchumbawako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa . Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako,na nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako.   Naamini sala hii kwako wewe mama mpenz sana haitapotea bure. Wew uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee   ili nijaliwe haya niombayo (   hapa omba hitaji lako unalota...

NOVENA YA MT RITHA WA KASHIA SIKU YA 9

Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Nina kuja mbele yako, Ee Mtakatifu Rita, siku hii ya mwisho ya Novena hii Takatifu. Ninayasikia mapigo ya moyo katika kipindi hiki kigumu cha maisha yangu yaliyogawanyika. Ninaamini kwamba ombi langu litatimizwa na Bwana kupitia maombezi yako Matakatifu. Lakini ikiwa haiwezekani,ninapaza sauti nikiomba kwanguvu huruma na faraja yako. Usiniache niondoke bila kupata faraja yako. Ee Mtakatifu Rita ,ninaomba unifariji kwa mastahili ya mateso uliyoyapata hapa duniani na katika upweke wako wa sala. Unifariji kwa mastahili ya ukarimu uliokua nao kwa wenye shida unisikilize kwa kwa mastahili ya upendo wako mkuu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa mama yake Bikira Maria Mtakatifu asiye na doa. Kwa mastahili ya ule mwiba Mtakatifu aliokujalia Bwana wetu Yesu Kristo,unisaidie na unifadhili mimi. Hiki ndicho kilio changu cha mwisho kwako wewe mama uliye Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa. Ninakuomba uj...