Litania Ya Huruma ya Mungu
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie. Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie. Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie. Kristu utusikie – Kristu utusikilize. Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie Mwana Mkombozi wa dunia Mungu – utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu – utuhurumie Utatu Mtakatifu Mungu mmoja –utuhurumie. Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu ~Tunakutumainia [KIITIKIO: Tunakutumainia] Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu. Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa. Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi. Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni. Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote. Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa. Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili. Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya d...