LITANIA KWA MT RITA WA KASHIA
Bwana
Utuhurukie, Kristo Utuhurumie, Bwana Utuhurumie,
Kiitikio ”Utuhurumie”
Baba wa
Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi
wa Dunia,Mungu, Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu,
Mungu Mmoja,
Maria Imakulata
Mama wa Mungu…………………….. Kiitikio
”Utuombee”
Maria, Mama
mfariji wa wanaoteseka Maria, Malkia wa Watakatifu wote Maria,
Mwombezi mpenzi
wa Mt Rita…………………….. Kiitikio
”Utuombee”
Mt Rita, Zawadi
toka Mbinguni …………………….. Kiitikio
”Utuombee” Mt Rita, Mwombezi
wetu mwenye nguvu: Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita,
mstaajabiwa tangu utoto wako: Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita,
Kielelezo cha usafi wa moyo: Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita,
kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita,
kielelezo bora cha mama mtaratibu: Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli: Mt
Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo
cha maisha ya kitawa: Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita,
mvumilivu wa kustajabiwa; Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi
katika kufanya toba; Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu
kwa masikini;
Mt Rita,
mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu; Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu
nzuri ya manemane; Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita,
mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita,
uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso; Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira
Maria;
Mt Rita, mwenye
kiu ya upendo wa Kimungu; Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya
mbinguni;
Mt Rita, utukufu
wa shirika la Mt Augustino; Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria; Mt Rita, mwenye
nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha
wa wanaopata mahangaiko; Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga
ya wokovu;
Mt Rita,
mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita,
mwombezi wa mambo yaliyoshindikana; Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada
wenye nguvu kwa wote; Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita,
uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
Mwanakondoo wa
Mungu uondoae dhambi za dunia, ”Utusamehe Bwana”
Mwanakondoo wa
Mungu uondoae dhambi za dunia, ”Utusikilize Bwana”
Mwanakondoo wa
Mungu uondoae dhambi za dunia ”Utuhurumie”
Kiongozi: Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: Kwa mhuli wa upendo na mateso Tuombe:
Ee Mungu ,
ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako
Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za
kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa
wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
Amina
Kila
baada ya kusali novena ya siku, tunasali litania hii kwa siku zote 12
Comments
Post a Comment