Posts

Litania Ya Huruma ya Mungu

Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie. Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie. Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie. Kristu utusikie – Kristu utusikilize.   Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie Mwana Mkombozi wa dunia Mungu – utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu – utuhurumie Utatu Mtakatifu Mungu mmoja –utuhurumie. Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu ~Tunakutumainia [KIITIKIO: Tunakutumainia]     Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu. Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa. Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi. Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni. Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote. Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa. Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili. Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya d...

LITANIA YA MOYO MTAKATIFU WA YESU

      Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie Utatu Mtakatifu Mungu mmoja Utuhurumie Moyo wa Yesu Mwana wa Baba wa Milele Utuhurumie Moyo wa Yesu uliotungwa na Roho Mtakatifu mwilini mwa Mama Bikira Maria Utuhurumie Moyo wa Yesu ulioungana na Neno wa Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu ulio na utukufu pasipo mfano Utuhurumie Moyo wa Yesu, hekalu takatifu la Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu, hema la Yule aliye juu Utuhurumie Moyo wa Yesu tanuru lenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, nyumba ya Mungu na mlango wa Mbingu Utuhurumie Moyo wa Yesu, tanuru yenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, chombo cha haki na upendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaojaa upendo na wema Utuhurumie Moyo wa Yesu, kilindi cha fadhila zote Utuhurumie ...

Litania ya Bikira Maria

Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie. Kristo utuhurumie. Kristo utuhurumie. Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie. Kristo utusikie. Kristo utusikilize Baba wa mbinguni, Mungu, utuhurumie. Mwana Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie. Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie. Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie. Kiitikio: Utuombee Maria Mtakatifu, Mzazi Mtakatifu wa Mungu, Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira, Mama wa Kristu, Mama wa neema ya Mungu, Mama mtakatifu sana, Mama mwenye usafi wa moyo, Mama usiye na doa, Mama usiye na dhambi, Mama mpendelevu, Mama mstaajabivu, Mama wa shauri jema, Mama wa Mwumba, Mama wa Mkombozi, Bikira mwenye utaratibu, Bikira mwenye heshima, Bikira mwenye sifa, Bikira mwenye enzi, Bikira mwenye huruma, Bikira amini, Kikao cha haki, Kikao cha hekima, Sababu ya furaha yetu, Chombo cha neema, Chombo cha heshima, Chombo bora cha ibada, Waridi lenye fumbo, Mnara wa Daudi, Mnara wa pembe, N...

LITANIA KWA MT RITA WA KASHIA

Bwana Utuhurukie, Kristo Utuhurumie, Bwana Utuhurumie, Kiitikio ”Utuhurumie” Baba wa Mbinguni, Mungu, Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu, Roho Mtakatifu, Mungu, Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,   Maria Imakulata Mama wa Mungu …………………….. Kiitikio ”Utuombee” Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka Maria, Malkia wa Watakatifu wote Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita …………………….. Kiitikio ”Utuombee” Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni …………………….. Kiitikio ”Utuombee”   Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu: Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu: Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako: Mt Rita, mpenda upweke: Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo: Mt Rita, kielelezo cha upole wote: Mt Rita, kielelezo cha mke mwema: Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu: Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli: Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia: Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa: Mt Rita, kioo cha utii; Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa; Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka; Mt Rita, shahid...

NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU KWANZA

Kwa jina la Baba,na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Mtakatifu Rita   mfanya miujiza,uniangalie kwa macho yako yenye huruma,mimi ninaye teseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu umezungukwa na miiba. Yaonr macho yangu, ee Mtakatifu Rita,kuwa hayatoki machozi tena kwani machozi mengi yamenitoka! Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu? Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu wa jina hilo, kwa kunijalia toka kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba    hitaji    lako    unalotaka    kumwomba Mungu    kupitia    Mtakatifu    Rita). Kila mtu anasifia utakatifu wako. Kila mtu anasimulia maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa njia yako. Je,mimi tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uni...

NOVENA MT. RIRHA WA KASHIA SIKU YA 2

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita wa Kashia.   Naona njia ya maisha yako imejaa majaribu na miiba mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua moyo wako vipande vipande. Ee Rita uliye kweli shahidi wa maumivu makali. Uliyeonja tone kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu makali. Nafikiria juu ya moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa maombezi yako   (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita). Wewe unajua maana ya moyo unaovuja damu. Unajua pia kifodini cha roho. Umeumizwa sana na kuteseka sana. Kwa njia ya mateso hayo nakuomba unisaidie katika mahangaiko yangu. Jesi kweli kwamba wakati huu mgumu, Bwana wetu Yesu ametuandalia njia ya kujipatia neema; kupitia miujiza ambayo binadamu wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi yako wakafanikiwa? Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako. Ninakutumainia, Ee Mta...

NOVENA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 3

Kwa jina la Baba,na la Mwana,na la Roho Mtakatifu.Amina Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa mapumziko,huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu,najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Ritha,unaye ng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za kanisa katoliki,natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini,kwa hamu nangojea,kupata kile nikiombacho   (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungi kupitia Mtakatifu Ritha) Nifikshie ombi langu kwa Yesu wa msalaba.Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopata majaribu,kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa,uliyomtolea Mungu wana wako,ukiomba wasinajisi...