Posts

Showing posts from August, 2025

JINSI YA KUSALI ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

ROZARI TAKATIFU YA MAMA BIKIRA MARIA Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.   Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk) .   Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.   Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika: “Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au; “Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee ...

Sala Kabla ya Kulala

  Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Wewe Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu ninayekutumaini.  Maana Wewe unaniokoa na mtego wa mwindaji na adui yangu, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya Yako unakufunika, Chini ya mbawa Zako nitapata kimbilio; Uaminifu Wako ni ngao na kigao. Sitaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pangu.  Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hawatanikaribia mimi kwa maana wewe unanilinda usiku huu. Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu Mabaya hayatanipata katika usiku huu, Wala tauni haitaikaribia nyumba yangu, Kwa kuwa utaniagizia malaika zako Wanilinde usiku huu na siku zote katika njia zangu zote. Mungu Baba naweka usiku huu juu yako, Asante kwa kunilinda. Naomba na Kushukuru kwa njia ya Kristu Yesu Bwana wetu. Amina Zaburi 19:1-10  

Kusali Rozari Nzima: Maana, Faida, na Jinsi ya Kusali

1. Maana ya Kusali Rozari Nzima Kusali Rozari Nzima kunamaanisha kusali Matendo(Siri) yote ishirini ya Rozari Takatifu, ambayo yamegawanyika katika sehemu nne: Matendo ya Furaha (Jumatatu & Jumamosi) Matendo ya Mwanga (Alhamisi) Matendo ya Huzuni (Jumanne & Ijumaa) Matendo ya Utukufu (Jumatano & Jumapili) Kwa kawaida, waamini husali sehemu moja ya Rozari kulingana na siku, lakini kusali Rozari Nzima maana yake ni kusali sehemu zote nne kwa pamoja, yaani jumla ya Salamu Maria 200, Baba Yetu 20, na Atukuzwe 20. 2. Faida za Kusali Rozari Nzima  Kuimarika kiroho – Rozari inatufanya tuwe na ukaribu na Mungu kupitia tafakari ya maisha ya Yesu na Maria.  Kufanikisha toba na wongofu – Kupitia tafakari ya mateso ya Yesu, tunapata neema ya kutubu dhambi.  Kukua katika fadhila – Rozari inatufundisha kuwa na subira, imani, upendo, na unyenyekevu.  Ulinzi dhidi ya majaribu – Mama Maria anatusaidia kushinda majaribu ya Shetani.  Kupokea rehema kwa dunia nzima – Ro...

NJIA YA MSALABA.

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.Amina. Tufwate njia ya msalaba, Tuifuwate, mpaka Kalvario. Tusimamepo, bila haya. Msalaba, Msalaba uponya roho. Sala mbele ya Altare Ee Mkombozi wangu, ninakuja Leo kufuata njia ile uliyoshika siku ya kufa sadaka yetu. Nimetubu dhambi zangu zote; ninataka kugeuza mwendo wangu, ninaomba kwako niwapatie roho za waumini marehemu waliomo toharani, rehema zote zilozotolewa na kanisa kwa Njia ya Msalaba. Nawe Maria Bikira Mtakatifu, uliyefuata njia ile nyuma ya mwanao Yesu, uniangalie kwa wema, unitie moyo mkuu, nisipende dhambi tena, nikivumilia kàzi na usumbufu na mateso na matukio yatakayonipata. Wimbo Umekosa nini we Yesu, Kushitakiwa bure kwa Pilato, Wenye kustahili hukumu, Si wewe, si wewe Bwana ni sisi. KITUO CHA KWANZA. Yesu anahukumiwa afe. Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru. Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu. Pilato anamhukumu Yesu ingawa haoni kosa lake, anawaogopa Wayahudi. Anabembeleza urafiki wa ...

NOVENA YA MT RITA WA KASHIA YA SAA 15 (SAA 9 - SAA 15)

MAALUM KATIKA SHIDA KUBWA SAA LA TISA (Sali Novena hii kila saa. Hadi ufikishe saa zote 15 bila kukatisha . Saa 15 za Novena hii hukumbuka miaka 15 ambayo Mt Rita aliishi na kidonda Katika Paji la uso wake Hadi kifo chake mwaka 1457) Ee Mungu chemichemi, huruma na msamaha ulimteua Mtumishi wako Rita wa Kashia ili awe mwombezi wa wote walio katika mahangaiko MAKUBWA. Nakuomba kwa maombezi yake yenye nguvu, neema ya kuondokana na shida hii KUBWA  ( hapa taja shida yako ) Bila maombezi yako Ee Mt Rita, siwezi kujinasua na shida hii KUBWA. Nakusihi uniombee kwa machozi yasiyokoma mbele ya Altare ya Mungu huko Mbinguni Mungu hakukatalii wewe kitu chochote kwani wewe ni Mtakatifu na mwombezi wa yote yaliyoshindikana kwa akili za kibinadamu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. Baba yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe x 3  SAA LA KUMI (Sali Novena hii kila saa.  Hadi ufikishe saa zote 15 bila kukatisha . Saa 15 za Novena hii hukumbuka miaka 15 ambayo Mt Rita aliishi na kidond...

NOVENA YA MT RITA WA KASHIA YA SAA 15 (SAA 1- SAA 8)

MAALUM KATIKA SHIDA KUBWA         *SAA LA KWANZA* (Sali Novena hii kila saa. Hadi ufikishe saa zote 15 bila kukatisha . Saa 15 za Novena hii hukumbuka miaka 15 ambayo Mt Rita aliishi na kidonda Katika Paji la uso wake Hadi kifo chake mwaka 1457) Ee Mungu chemichemi, huruma na msamaha ulimteua Mtumishi wako Rita wa Kashia ili awe mwombezi wa wote walio katika mahangaiko MAKUBWA. Nakuomba kwa maombezi yake yenye nguvu, neema ya kuondokana na shida hii KUBWA *( hapa taja shida yako )* Bila maombezi yako Ee Mt Rita, siwezi kujinasua na shida hii KUBWA. Nakusihi uniombee kwa machozi yasiyokoma mbele ya Altare ya Mungu huko Mbinguni Mungu hakukatalii wewe kitu chochote kwani wewe ni Mtakatifu na mwombezi wa yote yaliyoshindikana kwa akili za kibinadamu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. Baba yetu x 3 Salamu Maria x 3 Atukuzwe x 3   * SAA LA PILI* (Sali Novena hii kila saa. Hadi ufikishe saa zote 15 bila kukatisha . Saa 15 za ...

NOVENA YA MTAKATIFU YOSEFU ( SIKU YA 1-9)

SIKU YA KWANZA NIA YA MAOMBI Leo, tunapoanza novena hii, acha tuwaombe wanaume wote - ili wawe viongozi wakuu na walindaji waaminifu wa familia zao kama Mtakatifu Yosefu alivyokuwa. Acha pia tukumbuke wenzi wote wanaohusika katika sala zetu leo na kwa wale ambao wamegundua ndoa zao zina kisuko suko na wale wanaoomba kukutana na wenzi wa baadaye. TAFAKARI Yusufu alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru, akamchukua mkewe" (tazama Mt 1:24). Aliongozwa na Injili, baba wa kanisa kutoka karne za mwanzo alisisitiza kwamba kama vile Mtakatifu Yosefu alivyomtunza Maria na kujitolea kwa furaha kwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo, yeye pia anaangalia na kulinda mwili wa Kristo wa kihistoria, yaani, kanisa, ambayo Bikira Maria ni mfano na mfano. Yosefu wa Nazareti "alishiriki" [katika siri ya mwili] kama hakuna mtu mwingine isipokuwa Maria, mama wa neno la mwili. Alishirikiana naye pamoja naye; Alihusika katika tukio hilo la salvifi; Alikuwa mlezi wa upendo huo huo, kwa njia ...