NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 5
Kwa jina la baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu. Amina.
Ewe mchumba
mpendwa wa Yesu, Mtakatifu Rita wa Kashia; nakuja kwako tena. Nipo miguuni
pako. Navutwa na wema wako kwa Roho zenye kutaabika na kusumbuka. Unaona moyo
wangu ulivyo pondwapondwa kwa magumu ya dunia hii. Sipati tena tabasamu la
thanani, Roho yangu imevamiwa na mashaka mabaya. Imani imetetereka na mshituko
wa kukata tamaa kama msituko wa kifo unapiga miayo miguuni pangu. Nielekeze, Ee
Mtakatifu mpendwa nifanye nini katika mazingira haya ya kutisha? Nishauri
nimwendee nani katika hali ya hatari katika maisha yangu.
Kama kweli wewe
ni Mtakatifu wa hali zote za kukatisha tamaa, njoo unisaidie kwani najisikia
ninepotea. Nakuja kwako wewe ambaye kila mara wawahurumia wanaoteseka. Nakuja
kwako unisaidie. Je, hutanionea huruma kutokana na hali yangu? Mtakatifu Rita
najua u mwema sana. Najua hivyo , ndio maana najiweka mikononi mwako kwa moyo
wangu wote ili unijibu kwa njia ya Yesu, lile ombi langu ambalo kwa imani
naliomba ( hapa omba hitaji lako unalotaka kunwomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita )
Baba yetu (3), Salamu Maria (3), na
atukuzwe baba(3).
Kwa njia ya
Mtakatifu Rita: homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na
ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:watoto wanaomba
sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi
yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego
yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na
viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispania
wanakutangaza kuwa mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
fadhili zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu
mtakatifu, na kwa mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima,sifa za karne zote za
pendo la milele: Unawasaidia vipofu,
viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi : umemtia alama, Ee bwana ,
mtumishi wako Rita.
Wote : kwa muhuri wa upendo ma mateso.
TUOMBE:
Ee Mungu, uliyekubali
kumtawadha mtakatifu Rita kwa Neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi
akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.
Tunakuomba kupitia maombezi yake, Neema za kusamehe adui zetu na kutafakari
maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidi kwa wapole na wanao
teseka. Unayeishi na kutawala , daima na milele .Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia…….
(ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment