NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 4
Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu. Amina
Ee Mtakatifu wa
yale yaliyoshindikana,na wakili wa waliokata tamaa.Hizi ni sifa safi zenye
kujaa tumaini kwa roho zenye kujaribiwa na uchungu.Kwako wewe Mtakatifu Rita wa
kashia,ambaye wakati tunapojikuta pweke katika maisha yetu,tunapozungukwa na
huzuni na kifo,wewe watujia kama mtunza bustani kutoka mbinguni kutuletea ndani
ya mioyo yetu iliyokauka tumaini na maji
yaliyo hai.
Ee tumaini la
moyo wangu ulikauka kutokana na msongo mkubwa
wa huzuni;uzito wa maafa umenielemea,mashaka yananiogofya na sijui nielekee
wapi kutafuta msaada ninaohitaji.kwako wewe Rita mwema,ninakuamini sana na
kukutegemea;nakujia nikiwa na uhakika utanisikiliza. Kwa nguvu ya maombezi yako
mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,natumaini kusikilizwa katika ombi langu (hapa
omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)
Jionyeshe tena
kuwa u mwenye nguvu na huruma.Nithibitishie pia kuwa ni kweli kama wafuasi wako
wanavyokukili kuwa Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana, na wakili wa waliokata
tamaa.
Baba Yetu(3), Salamu Maria(3) na Atukuzwe
Baba(3).
Kwa njia ya
Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na
ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu,
viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi
yako;radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu.kwa utakatifu wako mitego
yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Hispania
wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako.Kashia hutukuza jina lako.
Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu
Mtakatifu,na kwa Mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za
pendo la milele. Unawasaidia
vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi : Umemtia alama, Ee
Bwana,mtumishi wako Rita. Wote :kwa mhuri wa
upendo na mateso.
TUOMBE:
Ee
Mungu,uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda
adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na
mateso.Tunakuomba kupitia maombezi yake,neema za kusamehe adui zetu na
kutafakari maumivu ya mateso yako,ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na
wananoteseka.Unaeishi na kutawala,daima n milele.Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia…….
(ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment