NOVENA YA MT. RITHA KASHIA NOVENA SIKU YA 8
Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mt. Amina
Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona
ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana,ninapotafakari paji la uso
wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka ktk taji la miiba la Yesu Kristo,
mchumbawako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni
mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake
akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa .
Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako,na
nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati
mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako. Naamini sala hii kwako wewe mama mpenz sana
haitapotea bure.
Wew uliye mfanya miujiza, mfadhili wa
mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa
mastahili ya pendo lako kwa Yesu
Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo ( hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Ritha) Mungu
hakukatalii wew kitu chochote; kwa maombezi yako,miujiza hufanywa,neema na
fadhila maalumu hupatikana. Hivyo, kwa moyo wangu wote na matumaini ya
dhati,ninasubiri nikitegemea kupata haya niliyoomba kwa Bwana Mungu.
Baba Yetu 3,
Salamu Maria 3 na Akukuzwe Baba 3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini
vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu,
viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina
nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari
kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na
viwete; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispani wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia
hutukuza jina lako ; Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba
sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na
heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi,
bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
Kiongozi : Umemtia alama Ee
Bwana, mtumishi wako Ritha.
Wote: Kwa muhuri wa upendo
na mateso.
Tuombe;
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu
Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na
katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake,
neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate
tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na
milele . Amina
Litania Kwa Mtakatifu
Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment