NOVENA MT. RITHA KASHIA SIKU YA 7
Kwa jina LA Baba, nala Mwana, nala Roho Mtakatifu . AMINA.
Ee mpedwa Rita, ambaye maisha
yako yalikuwa yahuzuni. Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu
makali. Naomba sala zangu, uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo
wako mpole ili uweze kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote
uliionesha kwa Jiran, maneno ya aman na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa
watu wote vinivute kukuelekea wewe uliye katika mbingu na unakoishi na kuwa
mwombezi wa watu wote waliokata tamaa.
Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo
kinarudi nyuma, vipofu wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza
wanaponyeshwa na ulemavu wote wa roho na mwili unaondoka kabisa. Je! Nipo peke
yangunjsiyefarijiwa na maombezi yako? Sitaamini wala siwezi kuamin hivyo. Nam
naamini kwa dhati usimamizi wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha
Mungu. Ninamatumaini makubwa kuwa nitapata amani, moyoni wang, utulivwana fadhila
ninazoomba nitajaliwa, [ hapa omba hitaji lako unalotaka
kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita]
Baba yetu×3, Salam
Maria×3, na Atukuzwe Baba×3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita~ homa,
madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
unawarudishia uhai.
Kwa maombezi yako~ radio,
tetemeko LA ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote,
hatari na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete ; watoto wanaomba sana na watu unawarudishia uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa
Mtakatifu wa mambo wa mambo yaliyoshindikana, watu wengi wanaimba sifa zako
Kashia hutukuza jina lako; Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto
wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, nakwa mwanae
ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia
vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia
uhai.
Kiongozi: Umemtia
alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa muhuri wa
upendo na mateso.
Tuombe:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha
Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohon
mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia
maombezi yako, neema za kusamehee adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso
yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa
Wapole na wanaoteseka. Unayeishi
na kutawala, daima na milele . Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa
Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment