NOVENA YA MT. RITHA WA KASHIA SIKU KWANZA
Kwa jina la Baba,na la Mwana na
la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee Mtakatifu Rita mfanya miujiza,uniangalie kwa macho yako
yenye huruma,mimi ninaye teseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu
umezungukwa na miiba. Yaonr macho yangu, ee Mtakatifu Rita,kuwa hayatoki machozi
tena kwani machozi mengi yamenitoka!
Nimechoka na kukata tamaa.
Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu?
Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu
wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu
wa jina hilo, kwa kunijalia toka kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba hitaji
lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita).
Kila mtu anasifia utakatifu wako.
Kila mtu anasimulia maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa njia yako. Je,mimi
tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uniombee kwa
Bwana Yesu ili anionee huruma na kunisaidia katika masumbuko na mahangaiko
yangu. Kwa maombezi yako, Ee Mtakatifu Rita,niweze kupokea kile ambacho moyo
wangu unatamani sana.
Baba yetu
×3 Salamu Maria
×3 na Atukuzwe
Baba ×3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:-
homa,madonda na tauni,viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke.
Unawasaidia vipofu , viziwi,
bubu na viwete :
watoto wanaomba sana
na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi,tetemeko
la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na
vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia
vipofu, viziwi, bubu
na viwete : watoto wanaomba
sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa
Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako . Kashia
hutukusa jina lako. Unawasaidia vipofu
, viziwi, bubu
na viwete : watoto
wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu na kwa Mwanae
ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele.
Unawasaidia vipofu , viziwi,
bubu na viwete :
watoto wanaomba sana
na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi : Umemtia alama Ee
Bwana,mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na
mateso.
TUOMBE
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha
Mtakatifu Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni
mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia
maombezi yake, neema za za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso
yako,ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na
kutawala,daima na milele. Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa
Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment