NOVENA MT. RITHA WA KASHIA SIKU YA 3
Kwa jina la
Baba,na la Mwana,na la Roho Mtakatifu.Amina
Natazama huku na
huko bila ya kupata mahali pa mapumziko,huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli
kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu
unaosononeka kwa uchungu,najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi
Mtakatifu Ritha,unaye ng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani
katika nguvu na nguzo za kanisa katoliki,natambua wewe unaimulika njia yangu
yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini,kwa
hamu nangojea,kupata kile nikiombacho
(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungi kupitia Mtakatifu Ritha)
Nifikshie ombi
langu kwa Yesu wa msalaba.Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako
ulipopata majaribu,kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa
hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza
kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa,uliyomtolea Mungu wana
wako,ukiomba wasinajisiwe kwa dhambi.Uniombee kwa Mungu.Hicho ni kifo dinicha
moyo wako.
Kupitia mateso
ambayo Bwana Yesu kristo aliruhusu yakupate ili utakaswe katika majonzi
yako,kwa njia ya majiribu mengi yaliyokupata na sadaka nyingi ulizotoa,uniombee
ili nijaliwe kupewa ombi langu ninalongojea kwa hamu.
Baba Yetu(3),salamu maria(3)na atukuzwe
Baba(3)
Kwa njia ya
Mtakatifu Ritha ;homa,madonda na tauni ,viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na
ghadhabu vitoweke umewasaidia
vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai kwa
maombezi yako;radi,tetemeko la ardhina moto havina nguvu.kwa utakatifu wako
mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na
viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai Hispania wanakutangaza
kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana.Watu wengi wanaimba sifa zako.Kashia
hutukuza jina lako unawasaidia
vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu
Mtakatifu,na kwa mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za
pendo la milele unawasaidia
vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi : umemtia alama,ee Bwana mtumishi
wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu
uliyekubali kutawadha Mtakatifu Ritja kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui
zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na
mateso.Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe adui zetu na
kutafakari maumivu ya metso yako,ili tupate tuzo uliotuhadia kwa wapole na
wanaoteseka.Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa
Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment