NOVENA MT. RIRHA WA KASHIA SIKU YA 2
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita
wa Kashia. Naona njia ya maisha yako
imejaa majaribu na miiba mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua moyo wako
vipande vipande. Ee Rita uliye kweli shahidi wa maumivu makali. Uliyeonja tone
kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu makali. Nafikiria juu ya
moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa maombezi
yako (hapa
omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Wewe unajua maana ya moyo
unaovuja damu. Unajua pia kifodini cha roho. Umeumizwa sana na kuteseka sana.
Kwa njia ya mateso hayo nakuomba unisaidie katika mahangaiko yangu. Jesi kweli
kwamba wakati huu mgumu, Bwana wetu Yesu ametuandalia njia ya kujipatia neema;
kupitia miujiza ambayo binadamu wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi
yako wakafanikiwa?
Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie
roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako. Ninakutumainia, Ee
Mtakatifu Rita. Niombee kwa Yesu mbinguni ili nipate kupokea yote ninayomwomba
Mungu kwa maombezi yako yenye nguvu.
Baba Baba Yetu (3), Salamu
Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:-
homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu
vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi,
bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi,
tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari
kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa
Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia
hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu,
viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa
Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la
milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu
na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi: Umemtia alama, Ee
Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na
mateso.
TUOMBE:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha
Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata
rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba
kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso
yako, ili tupate tuzo ulilotuahidi kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na
kutawala, daima na milele. Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)
Comments
Post a Comment