NOVENA YA MT RITHA WA KASHIA SIKU YA 9
Kwajina la Baba, na la
Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Nina kuja mbele yako, Ee Mtakatifu Rita, siku hii ya mwisho
ya Novena hii Takatifu. Ninayasikia mapigo ya moyo katika kipindi hiki kigumu
cha maisha yangu yaliyogawanyika. Ninaamini kwamba ombi langu litatimizwa na
Bwana kupitia maombezi yako Matakatifu. Lakini ikiwa haiwezekani,ninapaza sauti
nikiomba kwanguvu huruma na faraja yako. Usiniache niondoke bila kupata faraja
yako.
Ee Mtakatifu Rita ,ninaomba unifariji kwa mastahili ya
mateso uliyoyapata hapa duniani na katika upweke wako wa sala. Unifariji kwa
mastahili ya ukarimu uliokua nao kwa wenye shida unisikilize kwa kwa mastahili
ya upendo wako mkuu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa mama yake Bikira Maria
Mtakatifu asiye na doa. Kwa mastahili ya ule mwiba Mtakatifu aliokujalia Bwana
wetu Yesu Kristo,unisaidie na unifadhili mimi.
Hiki ndicho kilio changu cha mwisho kwako wewe mama uliye
Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa. Ninakuomba
ujidhihirishe katika mwanga wako halisi, ili Mungu anijalie haya ninayo yaomba.
(hapa
omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)
Kwa msaada wako ninadhamiria kuachana na mwenendo wangu
potofu, ili niwe muenezaji wa nguvu za Mungu na uzuri wa mambo ya Mbinguni.
Ninaahidi pia mahali pako pa upweke, Ee
Mtakatifu wa sala,huko Kashia,na au kwenye sanamu yako: ili niweze kuungana
nawe katika kuabudu na kushukuru kwa fadhila za Mbinguni nilizozipata kwa
maombezi yako kutoka kwa Mwokozi wetu Azizi Yesu Kristo. Baba Yetu 3, Salamu Maria 3, Atukuzwe 3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita : homa, madonda na tauni,viini
vya maradhi mbalimbali na ghadhabu vitoweke.
Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai .
Kwa maombezi yako: radi,tetemeko la ardhi na moto havina
nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote
hutoweka. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu
na viwete :watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mabo
yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako.Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:
watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu na kwa mwanae ziwe sifa,utukufu na
heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele.
Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai
Kiongozi : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote : Kwa mhuri wa upendo na mateso.
Tuombe:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa
neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika
paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema
za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako ili tupate tuzo
ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka . Unayeishi na kutawala, daima na
milele. Amina
Comments
Post a Comment