Litania ya Bikira Maria
Bwana
utuhurumie.
Bwana
utuhurumie.
Kristo
utuhurumie.
Kristo
utuhurumie.
Bwana
utuhurumie.
Bwana
utuhurumie.
Kristo utusikie.
Kristo
utusikilize
Baba wa
mbinguni, Mungu, utuhurumie.
Mwana Mkombozi
wa dunia, Mungu, utuhurumie.
Roho Mtakatifu,
Mungu, utuhurumie.
Utatu Mtakatifu,
Mungu mmoja, utuhurumie.
Kiitikio:
Utuombee
Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu
wa Mungu,
Bikira
Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa neema ya
Mungu,
Mama mtakatifu
sana,
Mama mwenye
usafi wa moyo,
Mama usiye na
doa,
Mama usiye na
dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama
mstaajabivu,
Mama wa shauri
jema,
Mama wa Mwumba,
Mama wa
Mkombozi,
Bikira mwenye
utaratibu,
Bikira mwenye
heshima,
Bikira mwenye
sifa,
Bikira mwenye
enzi,
Bikira mwenye
huruma,
Bikira amini,
Kikao cha haki,
Kikao cha
hekima,
Sababu ya furaha
yetu,
Chombo cha
neema,
Chombo cha
heshima,
Chombo bora cha
ibada,
Waridi lenye
fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya
dhahabu,
Sanduku la
Agano,
Mlango wa
mbingu,
Nyota ya
asubuhi,
Afya ya
wagonjwa,
Makimbilio ya
wakosefu,
Mfariji wa wenye
uchungu,
Msaada wa
Wakristu,
Malkia wa
Malaika,
Malkia wa
Mababu,
Malkia wa
Manabii,
Malkia wa
Mitume,
Malkia wa
Mashaidi,
Malkia wa
Waungama,
Malkia wa
Mabikira,
Malkia wa
Watakatifu wote,
Malkia
uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,
Malkia
uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari
takatifu,
Malkia wa amani.
Mwanakondoo wa
Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, utusamehe, Bwana.
Mwanakondoo wa
Mungu uondoaye dhambi za Ulimwengu, utusikilize, Bwana.
Mwanakondoo wa
Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, utuhurumie.
K. Utuombee,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe
ahadi za Kristu.
TUOMBE:
Ee Bwana Mungu,
utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na ya mwili sikuzote. Tuopolewe na
mashaka ya sasa kwa maombezi ya Maria mtakatifu, Bikira daima, ili tupate na
furaha ya milele.
Tunaomba hayo
kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
Comments
Post a Comment