Sala ya Ulinzi
Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila. Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili. Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose, Mintarafu matendo ya wanadamu; Kwa neno la midomo yako Nimejiepusha na njia za wenye jeuri. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa. Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.
Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako
wa kuume Uwaokoe nao wanaowaondokea. Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche
chini ya uvuli wa mbawa zako; Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho
yangu wanaonizunguka. Wameukaza moyo wako, Kwa vinywa vyao hutoa majivuno. Sasa
wametuzunguka hatua zetu, Na kuyakaza macho yao watuangushe chini. Kama mfano
wa simba atakaye kurarua, Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake. Ee
Bwana, usimame, umkabili, umwinamishe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu
mbaya.
Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li
katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana,
huwaachia watoto wao akiba zao, Bali mimi nikutazame uso wako katika haki,
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako Wewe Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji
ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za
haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako
vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka
mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili
zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
AMINA
Comments
Post a Comment