Malaika wa Bwana


Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.

Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Salamu, Maria,.....


Ndimi mtumishi wa Bwana.

Nitendewe ulivyonena.

Salamu, Maria....


Neno la Mungu akatwaa mwili.

Akakaa kwetu.

Salamu, Maria....


Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.

Tujaliwe ahadi za Kristu.


Tuombe

Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyon mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.

Amina

Comments

Popular posts from this blog

Litania Ya Huruma ya Mungu

LITANIA KWA MT RITA WA KASHIA

Kusali Rozari Nzima: Maana, Faida, na Jinsi ya Kusali