JINSI YA KUSALI ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA
ROZARI TAKATIFU YA MAMA BIKIRA MARIA
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika
taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa
Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti
kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na
ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk) .
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba
Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na
Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:
“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana
utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu
kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee
matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee
Bwana, Salamu Maria, …..” Au;
“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,…..
Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho
Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na
sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa
milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi.
Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio
unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…,
“Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele...” kama muda unatosha wimbo
ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja
uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe
kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama
inavyoonyeshwa hapa chini.
Comments
Post a Comment